- Mama huyo alijitia kitanzi akitumia kamba ya pasi baada ya sumu aliyokuwa ameinywa kukosa kumuua
- Barua ilipatikana chumbani mwa mama huyo ambapo alidai kwamba alikuwa amechoshwa na mateso ya mume wake
- Watoto hao wenye miaka saba na mitatu waliokolewa na majirani na kukimbizwa katika Hospitali ya Komarock Modern
Polisi katika kaunti ya Nairobi, wameanzisha uchunguzi baada ya mama mmoja kujitoa uhai usiku wa Jumatano, Mei 13, eneo la Komarock na kuwalisha wanawe wawili sumu.
Jane Mwende Nguthu, mwenye miaka 33, alijitia kitanzi akitumia kamba ya pasi baada ya sumu aliyokuwa ameinywa kukosa kumuua.
Habari Nyingine: Afisa wa polisi alazwa ICU baada ya kupigwa jiwe na raia aliyekiuka amri ya kafyu

Habari Nyingine: Magazeti ya Alhamisi, Mei 14: Wandani wa Ruto kuzindua kampeni dhidi ya Uhuru
Kulingana na taarifa ya polisi, barua ilipatikana chumbani mwa mama huyo ambapo alidai kwamba alikuwa amechoka kuteswa na mume wake.
Mume wake marehemu, aliwaambia maafisa wa polisi kwamba walikuwa wamekosana na hata kukosa kusemezana kwa siku moja.

Habari Nyingine: Kakamega: Mume ampiga na kumuua mkewe kwa sababu ya simu
Baba huyo alidai kuwa hakujua tofauti zao zingepelekea mke wake kutekeleza kitendo hicho.
Watoto hao wawili wenye miaka saba na mitatu waliokolewa na majirani na kukimbizwa katika Hospitali ya Komarock Modern ambapo wamelazwa huku wakiwa katika hali mahututi.
Kufikia sasa bado polisi hawajaweza kubaini aina ya sumu ambayo mama huyo aliwalisha watoto wake ambayo polisi walipata jikoni.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaoRxfJBmpJqlkWKuq7XTophmo5mprq%2FGyGaZmpmUlnq6rYykrLCZnJ7Aqa2MsJinmaeaenN50q6krmWbpLqivs6comegpKK5