Mtangazaji mkongwe wa Radio Citizen, Mohammed Juma Njuguna ameaga dunia. Habari za tanzia hiyo zimeripotiwa kupitia mmoja wa watangazaji wenzake wa muda mrefu redio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Royal Media Services.
Njuguna, 75, aliaga dunia mapema Jumamosi, Juni 8, akipokea matibabu katika Nairobi Hospital baada ya kuugua kwa muda wa wiki tatu ugonjwa wa kisukari.
Salamu za makiwa zinazidi kumiminika kufuatia kifo cha mtangazaji huyo ambaye alitangaza mpira kwa muda mrefu sana.
Alianzia utangazaji wake mbali kuanzia iliyokuwa Voice of Kenya, KBC na hatimaye Radio Citizen.
Anazikwa leo katika makaburi ya Karioko hapa jijini Nairobi.
Mengi kufuatia punde...
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZYR2f5hmpK2Znpyuu63JomSmo5%2BjtLixjLCYZqqRmbawecKiq6KylaN6rrvHmqSmnZRit7a5wGalo62XqruiecCanppllKq7qq2NoaumpA%3D%3D