Afisa wa polisi apiga mtindi hadi kujisahau, airusha bunduki yake barabarani

Posted by Larita Shotwell on Friday, September 20, 2024

- Kulingana na picha hizo zilizorushwa katika ukurasa mmoja maarufu wa Facebook, polisi huyo anaonekana kulewa chakari na kujisahau

- Picha za askari huyo ambazo TUKO.co.ke imeziona, zinaonyesha eneo linalosadikiwa kuwa kituo cha polisi ila hatuwezi kuthibitisha

- Kisa hiki kimezua maswali mengi kuhusu tabia ya baadhi ya maafisa wa polisi katika Huduma ya Polisi ambao kila mara wanaifanya huduma hiyo kuonekana isiyokuwa na nidhamu

Katika kisa cha kusikitisha afisa mmoja wa polisi amenaswa katika picha akiwa mlevi chakari aidha kwa pombe kali ambayo imemfanya kujisahau kabisa.

Kulingana na picha hizo zilizorushwa katika ukurasa wa Facebook, polisi huyo anaonekana ameketi kitako na bunduki yake ikiwa pembeni kabisa akijisikiza kabla ya kunyanyuka.

Habari Nyingine: Ngina Kenyatta na mabinti weingine 9 wa marais wa Afrika wanaopendeza ajabu

Katika kujinyanyua, ni wazi anakosa udhibiti wake na labda huenda alianguka wakati akiifikia bunduki yake.

Picha za askari huyo ambazo zinasambaa kwa kasi mtandaoni na ambazo TUKO.co.ke imezitizama, zinaonyesha eneo linalosadikiwa kuwa kituo cha polisi ila hatuwezi kuthibitisha hilo wala kusema kwa uhakika kilikuwa kituo gani lakini ni wazi alikuwa karibu na taasisi fulani.

Habari Nyingine: Eric Omondi ajifanya mganga Marekani, awanasa Wazungu wengi

Mavazi ya afisa huyo yanaonyesha ni wa kitengo cha Polisi Tawala na labda alikuwa akielekea kazini na akaona bora kupiga angalau glasi moja ya ‘chang’aa ama mratina’ lakini huenda alizidisha.

Kisa hiki kimezua maswali mengi kuhusu tabia ya baadhi ya maafisa wa polisi katika Huduma ya Polisi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiifanya huduma hiyo kuonekana mbaya zaidi.

Imeshangaza kwamba polisi anayefaa kuwasaidia Wakenya na kuwalinda kutokana na hatari anaweza kulewa jinsi hiyo.

Habari Nyingine: Picha 5 za Sheila Wetangula, bintiye seneta Moses Wetangula

Je huu ndio "UTUMISHI KWA WOTE"?

Wakenya wametoa maoni mbalimbali kuhusu kisa hiki na hapa ni baadhi ya maoni yao.

Habari Nyingine : Brazameni aliyedai kulala na wabunge 13 aibuka tena na ujumbe mtamu kwa Sabina Chege

Hùssein Yusuf hahaha leta iyo mtu apa Kismayu

Eng John Macharia Hapa ni wapi?

Angela Makau Why only focus on negativity yet these officers do alot of good things. Security starts with you

Christine Miheso Afanyiwe ibaada maalum akiwa sobre ataeneza gospel safi sana against kinywaji.

Patrick Barnabeu T M kenya pombe servicemen

Sam Kipchumba Is this serious...this are the guys we hear wsmeenda kuua bibi,watoto ama wenzake...he should hv been sacked like yesterday!

Habari Nyingine : Historia ya kupendeza kuhusu maisha ya Arnold ‘Commando’ Schwartzenegger

Mutsami Mutzz Shida wapi anakula jasho yake wewe nawe you are taking photos,you guys you are unfair mbona teachers,doctors,busness man/wemen etc when there are drunk you don't take photos why police?

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYBzhJdmmJ%2Bho5Z6uK2MqaaloaOeeqK8yKCYZqWknrultYyhmJ2hXaDCq7XSmp%2BarV2WtrPB0qGYZpqlo7G2t8hmsJqjlWKvor7Am5irmZ6ee6nAzKU%3D